February 12, 2026

MATIBABU YA FISTULA NA MSAMBA BURE – HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA BIHARAMULO

Tarehe: 20/02/2026 hadi 27/02/2026

Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania (AOFST) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Hospitali Teule ya Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera na Shirika la Fistula Foundation, wanatarajia kutoa matibabu ya fistula na kuchanika msamba katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo, kuanzia tarehe 20/02/2026 hadi tarehe 27/02/2026.

Matibabu haya ni BURE. Nauli na chakula vitatolewa kwa wagonjwa wote. Wakina mama wote wanaosumbuliwa na fistula ama waliochanika msamba wakati wa kujifungua kutoka katika mkoa wa Kagera na mikoa jirani mnakaribishwa kupata matibabu haya.

Karibu Tukurudishie Tabasamu

Karibu Tukurudishie Tabasamu

PIGA:
+255 764 185 018
+255 783 019 915

share on -